Somalia:Wanajeshi wa Kenya 'walionywa'

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Kenya waliouawa

Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia walionywa kuhusu shambulizi la kundi la Alshabaab siku 45 kabla ya kundi hilo kuvamia mojawapo ya kambi zao ,jenerali moja wa Somalia amesema.

Kenya ilipewa ripoti ya Intelijensi kuhusu tishio la uvamizi huo ,jenerali Abas Ibrahim Guery aliiambia BBC.

Wapiganaji hao wa kiislamu wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 katika shambulio hilo likiwa ni baya zaidi kuwahi kufanyika kwa jeshi la Kenya.

Image caption Mkesha wa kumbukumbu ya kuwanezi wanajeshi waliouawa nchini Somalia

Jeshi la Kenya bado halijatoa idadi ya wanajeshi waliouawa ama hata kujibu matamshi ya jenerali Gurey.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewatambelea baadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa katika hospitali ya Jeshi iliopo Nairobi kabla ya kuhudhuria hafla ya kuwakumbuka wanajeshi hao.