Wahamiaji 42 wazama baharini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahamiaji wengi hufanya safari hatari kuingia Ulaya

Takriban wahamiaji 42 wanaripotiwa kuzama baharini kwenye visa viwili katika bahari ya Aegean.

Mashua moja ilizama nje ya kisiwa kidogo cha Kalolimnos na kuwaua watu 34 wakiwemo watoto 11.

Watu wengine wanane walikufa baada ya mashua yao kuzama nje ya kisiwa cha Farmakonisi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Zaidi ya wahamiajia milioni moja waliingia ulaya mwaka uliopita

Zaidi ya wahamiaji milioni moja waliwasili barani Ulaya mwaka uliopita. Zaidi ya 700 walikufa katika bahari ya Aegean wakivuka kutoka Uturuki kwenda Ugiriki.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel hii leo anakutana na waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu mjini Berlin kuzungumzia suala hilo.

Siku wa Alhamis waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls alionya kuwa tatizo la uhamiaji barani ulaya linaiweka ulaya hatarini.