Misri yatofautiana na IS kuhusu shambulio

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Abdel Fattah al Sisi

Kundi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulio katika mji wa Cairo nchini Misri ambalo liliwaua takriban watu tisa wengi wao wakiwa maafisa wa polisi.

Lakini mamlaka imesema kuwa mlipuko huo ulitokea wakati wa uvamizi siku ya Alhamisi katika maficho yanayotumiwa na wapiganaji wa kundi la Muslim Botherhood.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shambulio Misri

Zaidi ya watu 13 walijeruhiwa akiwemo afisa mkuu wa polisi katika eneo la Giza,ambalo liko karibu na eneo maarufu lenye piramidi.

Serikali imeimarisha usalama huku taifa hilo likikaribia kuadhimisha miaka mitano ya mapinduzi yaliomuondoa rais wa muda mrefu wa taifa hilo Hosni Mubarak.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Vuguvugu la Muslim brotherhood,ambalo ndilo lililomuweka aliyekuwa rais Mohammed Morsi ambaye alichagliwa baada ya mapinduzi ilipigwa marufuku.