Myanmar yawaachilia wafungwa 100

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wafungwa Myanmar

Myanmar, inayofahamika pia kama Burma,inawaachilia wafungwa zaidi ya 100, wakiwemo baadhi waliofungwa kwa makosa ya kisiasa, wameeleza maafisa.

Hatua hiyo inakuja wiki moja kabla ya kukutana kwa serikali mpya kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa mwaka jana uliokuwa na ushindani mkali.

Miongoni mwa watakaoachiliwa ni Philip Blackwood, raia wa New Zealand alietumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kutusi imani ya Dudddha.

Blackwood alifungwa mwezi Machi kwa kutumia picha ya kuinadi baa.

Haijafahamika ikiwa wahudumu wake wawili raia wa Burma waliofungwa pamoja naye pia wataachiliwa huru .

Shirika lililoendesha kampeni za kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa linasema watu 52 waliopewa msamaha walikua ni wafungwa wa kisiasa.

Hukumu za wafungwa karibu 80 waliokuwa wamehukumiwa kifo pia zimebatilisha na sasa watafungwa kifungo cha maisha.

Msemaji wa rais Zaw Htay amesema kwenye mtandao wake wa Facebook kwamba jumla ya wafungwa 102 wanaachiliwa leo.