Sudan yaipunguzia ada Sudan Kusini

Image caption Sudan Kusini hulazimika kutumia mabomba ya mafuta ya Sudan kuweza kuuza mafuta yake nje

Sudan imekubali kupunguza ada inayotosa jirani wake Sudan Kusini kusafirisha mafuta kupitia kwa mabomba yake.

Nchi zote mbili zimekuwa zikitofautiana kuhusu ada hiyo ambayo imetishia kuangamiza sekta ya mafuta ya Sudan Kusini baada ya mzozo wa hivi majuzi.

Wakati Sudan Kusni ilipopata uhuru wake pia ilipata maeneo yenye utajiri wa mafuta lakini huwa inalazimika kutumia mabomba ya mafuta ya Sudan kuweza kuuza mafuta yake nje.

Ada inayotoswa na Sudan kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini ni dola 24 kwa pipa, na wakati bei ya sasa ya mafuta ni dola 30 kwa pipa, suala hilo limeiathiri pakubwa Sudan Kusini.