Mwanafunzi Mmarekani akamatwa Korea Kaskazini

Korea Haki miliki ya picha EPA
Image caption Uhusiano kati ya Korea Kaskazini na nchi za Magharibi umeendelea kudorora

Korea Kaskazini imesema imemkamata mwanafunzi kutoka Marekani ambaye anadaiwa kufanya “kitendo cha uchokozi” dhidi ya taifa.

Shirika la habari la serikali KCNA limesema serikali ya Marekani ilikuwa “imemvumilia na kumtawala kwa werevy” mwanafunzi huyo, ambaye husomea Chuo Kikuu cha Virginia.

Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halijatolewa anadaiwa kuingia Korea Kaskazini kama mtalii, na inadaiwa “alilenga kuvunja umoja wa taifa hilo”.

KCNA haijatoa maelezo zaidi, lakini mwanafunzi huyo anaendelea kuchunguzwa.

Afisa wa ubalozi wa Marekani katika taifa jirani la Korea Kusini ameambia shirika la habari la Reuters kwamba hawana habari kuhusu kukamatwa kwa mwanafunzi huyo.

Ikithibitishwa, basi mwanafunzi huyo atakuwa wa tatu kutoka nchi za Magharibi kuzuiliwa nchini Korea Kaskazini.

Mhubiri kutoka Canada na mwanamume mwingine Mkorea-Mmarekani pia wanazuiliwa na maafisa wa taifa hilo.