Sina Weibo kuongeza kiwango cha ujumbe

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sina Weibo

Mtandao maarufu wa Uchina Sina Weibo,umeamua kuongeza idadi ya herufi na nambari pamoja na viasharia ambavyo wateja wake wanaweza kuandika katika ujumbe mmoja.

Kufikia sasa mtandao huo wa kijamii ulikuwa ukitumia herufi 140 pekee katika ujumbe.

Lakini kuanzia tarehe 28 mwezi Januari,utawaruhusu baadhi ya watumiaji wake kuandika ujumbe mrefu ijapokuwa sio ujumbe wote utaonekana mara moja.

Hatua hiyo huenda ikatoa shinikizo kwa mtandao wa tweeter kuiga mfano huo.

Shirika la habari la Uchina Xhinua limeripoti kwamba Mkuu wa mtandao huo Wang Gaofei amethibitisha hatua hiyo.

Limesema kwamba katika jaribio la kwanza wateja wataona kiwango cha herufu 140 ,lakini watalazimika kubonyeza ili wapate huduma hiyo ya kutuma ujumbe mrefu.

Umeongezea kwamba ni watu wazima pekee watakaoweza kutumia huduma hiyo mara moja lakini itakuwa wazi kwa watumiaji wengine kabla ya mwisho wa mwezi Februari.

Mtandao wa Weibo unadaiwa kuwa na watumiaji milioni 200.