Wanne wauawa katika ufyatulianaji risasi Canada

Haki miliki ya picha AP
Image caption Eneo la tukio la ufyatulianaji wa risasi nchini Canada

Polisi nchini Canada wamesema kuwa watu wanne wameuawa katika ufyatulianaji wa risasi katika shule moja katika Mkoa wa Saskachewan, katikati mwa Canada.

Ripoto za awali zilikuwa zimesema ni watu watano waliofariki.

Mshukiwa mwanamume ametiwa mbaroni nje ya Shule ya Kijamii ya Loche, ambako kisa hicho kilitokea.

Polisi pia wanaendelea kufanya uchunguzi katika tulio jingine la ufyatulianaji risasi katika kijiji cha watu 3,000 nchini humo.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudea, ametaja vifo hivyo kama hofu kubwa inayoweza kumkumba mzazi yeyote.

Mauaji ya watu wengi kwa bunduki nchini Canada si jambo la kawaida , ambako sheria za kuthibiti bunduki ni kali zaidi kuliko Marekani.