Google kuilipa UK kodi ya dola milioni 200

Haki miliki ya picha
Image caption Google

Kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Google imekubali kulipa karibu dola milioni 200, kama kodi ya mwongo mmoja kwa Uingereza.

Kampuni hiyo imelaumiwa mara kadhaa kwamba inakwepa kulipa ushuru licha ya kuunda mabilioni ya Dola kutoka biashara yake ya mauzo nchini humo.

Wakosoaji wanasema kiasi hicho ni kidogo sana na kwamba ikilinganishwa na biashara na mapato yake ya kila mwaka walistahili kulipa kiasi kikubwa zaidi.

Google ni mojawapo ya kampuni kubwa zilizomulikwa na mataifa kadhaa kwa madai ya kukwepa kodi kwa njia zisizoeleweka.