Uhispania:Waziri Mkuu akataa kuunda serikali

Haki miliki ya picha diariopontevedra
Image caption Waziri mkuu wa Uhispania Mariana Rajoy

Waziri Mkuu wa muda wa Uhispania amekataa ombo la kuunda Serikali mpya.

Bwana Rajoy, ambaye chama chake kisichopendelea mabadiliko cha Popular Party kilishinda viti vingi vya Bunge, bila kuwa na idadi ya kutosha ya kuunda Serikali, katika uchaguzi wa mwezi uliopita, alikataa ombi la Mfalme Filipe kuwa aunde Serikali.

Kwa mara ya kwanza tangu demokrasia irejee nchini Uhispania, Mfalme alikuwa mwenyekiti wa mkutano ulioshirikisha vyama vya kisiasa vinavyopingana.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pedro Sanchez

Ana nia ya kumaliza hali ya kutoafikiana katika kuunda Serikali.

Waandishi wanasema kuwa huenda Mfalme huyo akamsihi kiongozi wa chama cha kisosholisti Pedro Sanchez kuunda serikali mpya.