'Viongozi wa ANC ni mafisadi'- Goldberg

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waondoeni viongozi wote wa ANC ni Mafisadi, asema Goldberg

Mwanaharakati maarufu wa Afrika Kusini, Denis Goldberg, ametoa wito kuwa viongozi wa chama tawala cha ANC, waondoshwe madarakani.

Bwana Goldberg alifikishwa mahakamani pamoja na Nelson Mandela, na kutumikia kifungo cha miaka zaidi ya miaka 20 jela.

Lakin baada ya tathmini yake ya hali ya kisiasa ilivyo nchini Afrika Kusini, bwana Goldberg ameiambia idhaa ya BBC kuwa daraja zote za uongozi wa ANC, kutoka majimboni hadi ngazi za taifa, umehusika na rushwa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Goldberg anasema tamaa ya viongozi wa ngazi zote za ANC za kujilimbikizia mali inawanyima raia wa Afrika Kusini uhuru

Kigogo huyo wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa ,alisema lengo lao la kujitajirisha kwa haraka kumewanyima wa-Afrika Kusini uhuru wao.