Zika:Brazil yatoa hakikisho

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zika:Brazil yatoa hakikisho

Utawala mjini Rio de Janerio umetangaza mipango yake ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Zika wakati wa mashindano ya olimpiki baadaye mwaka huu.

Mlipuko wa ugonjwa huo unaosambazwa na mbu ambao unaweza kusababisha madhara makubwa kwa watoto wanaozaliwa umasababisha hofu kubwa nchini Brazil.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ugonjwa wa Zika unasababisha watoto kuzaliwa wakiwa na kichwa kidogo

Ili kuwahakikishia usalama mamilioni ya watu ambao watahudhuria mashindano hayo.

Maafisa wanasema kuwa ukaguzi wa vifaa vya mashindano hayo utaanza miezi minne kabla ili kuhakikisha kuwa hakuna mazingira salama kwa mbu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Zika huambukizwa na mbu

Wizara ya afya nchini Brazil inasema kuwa miezi ya Julai na Agosti ambapo mashindano hayo yatafanyika huwa na kibaridi na kwamba hayatakuwa mazingira salama kwa mbu.