Burkina Faso: Wanajeshi waiba silaha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Burkina Faso: Wanajeshi waiba silaha

Jeshi nchini Burkina Faso linasema kuwa takriban wanajeshi 10 wamekamatwa baada ya kuhusishwa na uvamizi kwenye ghala la zana za vita nje ya mji mkuu Ouagadougou.

Jeshi lilisema kuwa wale wote waliokamatwa walikuwa wanachama wa zamani wa kikosi cha kumlinda rais ambacho kilivunjwa mwezi Septemba baada ya mapinduzi yaliyofeli.

Kikosi hicho kilikuwa watiivu kwa rais wa zamani Blaise Compaore ambaye alipinduliwa mwaka 2014.