Jordan yawaua wavamizi 12 mpakani

Haki miliki ya picha
Image caption Jeshi linasema kuwa lilipata tembe milioni mbili za madawa wakati wa kisa hicho.

Jordan inasema kuwa walinzi wake wa mpaka wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 12 baadhi yao waliokuwa wamejihami.

Wavamizi hao walikuwa miongoni mwa kundi la karibu watu 30 waliojaribu kuingia nchini hu,o wakitokea nchini Syria.

Jeshi linasema kuwa liliwasimamisha mara kwa mara watu waliotaka kuvuka mpaka lakini limetaja tukio la ufyatulianaji wa risasi wa siku ya Jumamosi kuwa kisa kibaya zaidi kuwahi kutokea.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jordan yawaua wavamizi 12 mpakani

Jeshi linasema kuwa lilipata tembe milioni mbili za madawa wakati wa kisa hicho.

Jordan imewapokea maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Syria lakini imedhiditi zaidi mipaka yake hivi majuzi ikisema kuwa ina hofu kuwa makudi yenye siasa kali yataingia nchini humo.