Misri na mgogoro wa kibinaadam

Haki miliki ya picha BBC World Service

Shirika la kimataifa la kutetea haki za bimaadamu Amnesty International, linasema nchi ya Misri inasumbuliwa na suala la mgogoro wa haki za kibinadamu kwa kiwango kikubwa ,na haya ni matokeo ya miaka mitano baada ya maandamano yaliyomn'goa raisi Hosni Mubarak.

Kikundi kimoja cha cha kampeni kinasema kuwa siku za hivi karibuni idara ya usalama imeamua kuvamia nyumba zipatazo elfu tano mjini Cairo ili kuwabaini watu waliopanga njama za kuandamana hii leo katika kumbukumbu ya kung'olewa kwa Mubarak.

Shirika la Amnesty linasema jeshi la Polisi la taifa hilo la Misri linakiuka wajibu wake kwa kuwakamata wanaharakati wengi au kuwafanya wengi kujificha ili kupiga marufuku maandamano hayo kufanyika.