Tetemeko la ardhi lakumba Morocco

Haki miliki ya picha Deepak Shijagurumayum
Image caption Maktaba: Tetemeko la ardhi lakumba Morocco

Tetemeko kubwa la ardhi lenye uzito wa 6 nukta moja 1 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Mediterranea kati ya Morocco na Uhispania, na kusababisha hasara.

Hayo ni kwa mjibu wa Idara ya Jiologia ya Marekani, (USGS).

Tetemeko hilo lilitokea katika eneo hilo mwendo wa saa kumi u nusu alfajiri, kilomita 62 Kaskazini mwa mji wa Al Hoceima nchini Morocco, kilomita 164 kusini mashariki mwa mji wa Gibraltar.

Tetemko hilo lilifuatiwa na linginge lenye uzito wa 5 nukta 3 katika kipimo cha Richter.

Idara hiyo ya USGS imetoa taarifa ya awali ikisema kuwa, huenda hakujatokea maafa ila hasara kidogo.

Zaidi ya watu 630 waliuwawa mwezi Februari mwaka 2004, pale tetemeko baya lenye uzito wa 6 nukta 3, lilipotokea karibu na mji wa Al Hoceima.