Je Wema kapata mchumba ?

Image caption Je mpenzi wa zamani wa Diamond Platinumz bi Wema Sepetu kapata mchumba?

Je mpenzi wa zamani wa Diamond Platinumz bi Wema Sepetu kapata mchumba?

Kulingana na ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother Idris Sultan,

Wema sio tu eti keshapata mchumba ila pia ashapata uja uzito!

Idris, ambaye alikuwa amehusishwa na totoshoo huyo kwa muda mrefu alikuwa akibubujikwa na penzi katika taarifa hiyo yake kwenye Instagram.

''Mimi nawe sio wa kawaida. Nala, natembea, nalala, nazungumza nikikuwazia wewe tu.''

''Na kama utadhani kuwa umebahatika kuwa nami, pia mimi naona nimebahatika kuwa nawe.''

Image caption Idris Sultan (IG)

''At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama.''

“Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike”.

''Au ukiingia jikoni kwangu na unapika na kuniandalia chakula kizuri,” aliandika Idris.

“Nitafanya kila niwezalo ilimradi ufurahi.

''Nitakulinda, nikupende, nikutendekeze, tupike nawe, tujiburudishe kwa pamoja na kujivinjari; kwa hakika wewe ndiye uliyekonga moyo wangu''.

''Wewe ndiye mke wangu''.

Image caption Mchumba wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum amepata mtoto na bi. Zari kutoka Uganda ambaye ni mpinzani mkubwa wa Wema.

Idris na Wema watakumbukwa kwa kuanda matangazo ya kibiashara kama ''mume na mkewe''

Wema kwa upande wake alimsifu Idris kwa ucheshi wake hata mara nyengine akiachilia picha zake kwenye mtandao wake wa Instagram na kumtambua kama ''mpenzi''

Wema alitofautiana na Diamond Platinumz na akakurubiana na mwakilishi mwengine wa Big Brother Luis Munana raia wa Namibia.