EU na suala la wakimbizi

Haki miliki ya picha Getty

umoja wa ulaya umekaribia kukubaliana juu ya makubaliano ya Schengen katika suala la kufungua mipaka baina yao kusitishwa mpaka baada ya miaka miwili kutokana na kufurika kwa wahamiaji na wakimbizi .Katika kikao cha mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za ulaya huko Amsterdam kilichoibuka na mapendekezo kuwa Ugiriki inapaswa kutengwa katika jumuiya ya schengen kama haitaweza kufuata masharti yaliyowekwa.

Waziri wa uhamiaji wa Ugiriki,Yiannis Mouzalas alisisitiza kuwa nchi yake inafanya kila iwezalo ili kutatua tatizo la madeni yanayowasakama.Ugiriki imechoka kusikia kuwa mipaka yao haitalindwa kwa sababu ya madeni.

Umoja wa ulaya inasema ni takribani waamiaji zaidi ya elfu mbili wanaingia Ugiriki kila siku licha ya kwamba kuna bahari na kuna hali ya hewa ya kipupwe kikali.