Raia walazimika kula matunda mwitu Msumbiji

Image caption Ukame nchini Msumbiji

Mamlaka ina wasiwasi kuhusu ukame unaoathiri takriban watu 170,000 kusini na katikati mwa nchi ya Msumbiji.

Ukosefu wa maji umewaua zaidi ya ng' ombe 3,000 na mbuzi ambao kwa sasa wanakabiliwa na ukosefu wa nyasi.

Kitengo cha maswala ya misaada pamoja taasisi inayokabiliana na majanga zimesema kuwa baadhi ya raia katika jimbo la Inhambane ambapo watu 70,000 wameathirika, wanaishi kwa kutumia matunda mwitu.

Mamlaka ya taifa hilo inasema kuwa watu hawapati msaada wa chakula cha kutosha ili kukimu mahitaji yao.