Mamia wadai ushindi wa $47m za Lotto

Image caption Mamia wadai ushindi wa $47m za Lotto

Mamia ya raia wa Uingereza walioshiriki katika mchezo wa bahati nasibu wenye zawadi ya $47m ama pauni milioni 33.

Kwa mujibu wa waandalizi wa mchezo huo wa bahati nasibu Camelot wamepokea mamia ya malalamishi kutoka kwa watu wanaodai wao ndio walionunua tiketi hiyo ya bahati ambayo hadi sasa mshindi hajajitokeza.

Mamia ya watu wanadai kuwa waliiosha tiketi hiyo wengine wanasema kuwa waliipoteza huku mama mmoja akidai kuwa ndiye aliyenunua tiketi hiyo ila ikaibiwa.

Kwa mujibu wa Camelot tiketi iliyoshinda iliuzwa katika kitongoji cha Worcester.

Kitita hicho cha pauni milioni 33 ilikuwa sehemu ya zawadi ya pauni milioni 66 aliyokuwa ikishindaniwa katika droo kubwa ya kufungwa msimu iliyofanyika tarehe 9 mwezi Januari.

Nambari mbili za tiketi zilichaguliwa huku wakitarajiwa kugawanya pauni milioni 33 kila mmoja.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Washindi wa kwanza mume na mkewe ambao ni wenyeji wa mji mdogo wa Hawickwho,walijitokeza na kuchukua zawadi yao ya pauni milioni 33

Washindi wa kwanza mume na mkewe ambao ni wenyeji wa mji mdogo wa Hawickwho,walijitokeza na kuchukua zawadi yao ya pauni milioni 33 na sasa harakati za kumtafuta mshindi wa pili zikiendelea.

Hadi kufikia sasa jina la mshindi huyo halijatangazwa na vilevile duka ilikouzwa.

Camelot inasema ingali inafanya uchunguzi kubaini njia mbadala za kuthibitisha aliyenunua hati hiyo ya bahati.

Kwa mjibu wa msemaji wa kampuni hiyo, Camelot inaweza kumzawadi mtu anayewaandikia barua katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja tangu ya kufanyika droo ima ataelezea kuwa hati yake imepotea imeibiwa ama hata imeharibika.

Muuzaji mmoja bwana Natu Patel, ambaye huuza hati za bahati mjini Worcester,mama mmoja alikwenda kwake kudai tuzo hilo la kihistoria ila tiketi yake ilikuwa imeharibika mno.

Ticketi yenye nambari 26, 27, 46, 47, 52 58 ndiyo ya mshindi wa pauni milioni 33.

Hii ndio zawadi ya juu zaidi kuwahi kutolewa kwa mshindi katika historia ya mchezo wa bahati na sibu iliyozinduliwa mwaka wa 1994.