Papa Francis awaomba radhi Waprotestanti

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Papa Francis

Katika hatua ya kujumuisha umoja wa kikristo, Papa Francis amewaomba radhi waumini wa Kiprotestanti kutokana na unyanyasaji walioupata kutoka kanisa Katoliki miaka ya nyuma.

Papa Francis amewataka waumini wa kanisa Katoliki pia kuwasamehe wale ambao waliwakosea ili wasiruhusu makosa yaliyotendeka nyuma kuwa sumu ya mahusiano ya sasa. Kufuatia tamko hilo msemaji wa Vatcan ametangaza kuwa Papa Francis atazuru mji wa Lund uliopo Swedish eneo ambalo jumuiya ya Kilutheri ilianzishwa na kuanzisha thehebu la Kilutheri karne tano zilizopita.