Senegal yapambana na ugaidi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Polisi nchini Senegal

Polisi nchini Senegal wamewakamata watu wapatao mia tisa katika kamata kamata ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na ugaidi.

kamata kamata hiyo ilifanyika mwishoni mwa juma katika mji mkuu wa Dakar karibu na mtaa wa Thies.Jeshi la ulinzi wametoa angalizo tangu shambulio lililowahi kutokea mapema mwezi huu katika hoteli iliyoko mji mkuu wa Burkina Faso,ambapo watu thelathini waliuawa .

wiki iliyopita waziri wa mambo ya ndani Abdoulaye Daouda Diallo alizitaka hoteli zote nchini humo kuongeza ulinzi.