Utoaji mimba Sierra Leone wapingwa

Haki miliki ya picha GETTY

Viongozi w Kikristo na kiislamu nchini Sierra Leone wameandamana hadi katika majengo ya Bunge katika mji mkuu wa Freetown kupinga muswada wa sheria unaoruhusu utoaji wa mimba.

Mwandishi wa habari wa BBC amesema mamia wamejitokeza katika maandamano hayo. Viongozi hao wa dini wamesema Sheria ya utoaji mimba salama, inayoruhusu wajawazito wa hadi wiki kumi na mbili kutoa mimba inakwenda kinyume na vitabu vitakatifu vya Biblia na Koran.

Wanaharakati wanaounga mkono sheria hiyo wanasema utoaji halali wa mimba utapunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua wakiwa chini ya madaktari wasio na ujuzi.

Bunge lilipitisha mswada huo mwezi Decemba mwaka jana lakini Rais wa nchi hiyo Ernest Bai Koroma alikataa kuusaini kuwa sheria baada ya kufuatwa na viongozi wa dini.