Wanajeshi waliofariki wakumbukwa Kenya

Image caption Wanajeshi wakiwa shada la maua katika eneo la kumbukumbu za wanajeshi waliofariki

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari pamoja na mwenzake wa Somalia Hassan Mohamoud tayari amewasili katika mji wa Eldoret nchini Kenya kwa kumbukumbu ya heshima za wanajeshi wa Kenya waliouawa nchini Somalia.

Image caption Eneo la kumbukumbu

Marais wote wawili walilakiwa na mwenyeji wao Uhuru Kenyatta wa Kenya .

Mtandao mmoja wa serikali ulituma ujumbe wa picha ya ndege ya rais Mohamoud Buhari ilipotua katika uwanja wa ndege wa Eldoret ambapo raia wanangoja kuanza kwa hafla hiyo.

Image caption Wanajeshi wakijiandaa

Wanajeshi hao waliuawa na wapiganaji wa Alshabaab katika kambi yao ya el-Ade nchini Somalia mnamo tarehe 15 mwezi Januari.

Image caption Wanajeshi waliofika

Tayari maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika.