Mauzo ya iPhone yapungua duniani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mauzo ya simu ya Iphone yapungua

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple imeripoti kupungua kwa mauzo ya simu za iPhone katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho mwaka uliopita.

Kampuni hiyo iliuza simu milioni 75 mwaka uliopita ikiwa ni mauzo ya chini zaidi tangu mwaka 2007.

Hii ni kutokana na kuyumba kwa uchumi wa China.

Hata hivyo faida ya kampuni ya Apple iliongezeka katika kipindi hicho kwa zaidi ya dola bilioni 18.

Mhariri wa masuala ya Teknolojia katika mtandao wa CNET Ian Sherr, amesema huenda soko la simu za mkononi limefurika.