Malaysia:Wataka kukata rufaa dhidi ya Razak

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Najib Razak

Shirika la kukabiliana na ufisadi nchini Malaysia linasema kuwa litakata rufaa kuhusu uamuzi wa kuondoa tuhuma za ufisadi dhidi ya waziri mkuuu, Najib Razak.

Waziri mkuu huyo alidaiwa kupokea mamilioni ya dola kiharamu.

Siku ya jumanne, mkuu wa sheria alisema uchunguzi haukupata ushahidi kwamba Bw. Najib alivunja sheria.

Alipokea karibu dola milioni mia saba kutoka kwa familia moja nchini Saudi Arabia, kabla ya uchaguzi mwaka 2013.

Kesi hiyo imetikisa nchi hiyo na kutishia kumtoa madarakani. Uamuzi wa kumuondelea mashtaka umezua hisia kali.