Chris Brown aondolewa mashtaka Las Vegas

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chris Brown aondolewa mashtaka Las Vegas

Muimbaji maarufu wa muziki wa kizazi kipya Chris Brown ameondolewa lawama yawizi na kupigana na utawala wa Las Vegas Marekani baada ya mwanamke mmoja kudai alimzaba kofi na kumpokonya simu yake walipokutana kwenye Kasino moja ya kamari mapema mwezi huu.

Mkuu wa sheria katika jimbo hilo Steve Wolfson amesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia msanii huyo mashtaka ya utovu wa nidhamu kwa kumshambulia mwanamke huyo na kumuibia simu .

Msemaji wa Brown alikanusha madai ya mwanamke huyo akisema kuwa sio ya kweli hata kidogo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwaka 2009, Brown alipatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna

Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa lolote baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna.