Toyota yaongoza kwa mauzo duniani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kampuni ya magari ya Toyota

Toyota inaendelea kuongoza kama kampuni inayotengeza magari kwa mwaka wa nne mfululizo.

Kampuni hiyo iliuza magari milioni 10.15 kwa jumla mwaka 2015 na kuvunja rekodi ya matarajio ya wengi.

Kampuni ya Ujerumani ya Volkswagen imekuwa ya pili ikiwa imeuza magari milioni 9.93,ikifuatiwa na General Motors kutoka Marekani iliouza magari milioni 9.8.

Volkswagen ilikuwa inaongoza nusu ya mwaka wa 2015 kabla ya kashfa ya magari yake kutoa moshi mchafu kupunguza mauzo yake.

Biashara katika masoko makubwa kama vile Marekani na Japan na masoko yanayoinuka imepungua kutokana na kuanguka kwa uchumi duniani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Toyota

Mwaka 2014,Toyota iliibuka kidedea kwa kuuza magari milioni 10.23.

Kampuni hiyo imepata sifa kwa magari yake aina ya Prius hybrid,Camry,Corolla Sedan na Lexus.