Ugaidi:Waziri wa haki ajiuzulu Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi. Taubira kulia

Waziri wa haki nchini Ufaransa Christiane Taubira amejiuzulu mda mfupi kabla ya wabunge kujadili mpango wa kuwapokonya uraia waliopatikana na hatia ya ugaidi.

Bi. Taubira alidaiwa kukataa mapendekezo hayo.

Mpango huo ulipendekezwa baada ya shambulio la kigaidi la Zeptemba 13 mjini Paris ambapo watu 130 waliuawa.

''Wakati mwengine kuendelea kukataa ni sawa na kupinga ,lakini pia mara nyengine kukataa inamaanisha kuondoka'',alituma ujumbe wake katika mtandao wa tweeter.

Mahala pake taubira pamechukuliwa na Jean,Jacques Urvoas.