Zika: Obama ataka hatua za haraka kuchukuliwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Barrack Obama

Rais wa Marekani Barack Obama ameomba hatua za haraka katika kufanya majaribio ya chanjo na kutafuta tiba dhidi ya virusi vya Zika.

Virusi hivyo vinaambukizwa na mbu na vinasababisha dosari za maumbile, ambapo watoto wanazaliwa wakiwa na vichwa vidogo.

Bw Obama amepokea taarifa kuhusu mulipuko wa Zika na kuna hatari Marekani ikakumbwa na visa vya virusi hivyo katika msimu wa joto.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Virusi vya zika

Rais ametaka raia wa Marekani kupata taarifa ya jinsi ya kujikinga na maambukizi hayo.

Jumanne ya wiki hii mkaazi wa jimbo la Virginia alipatikana na virusi hivyo baada ya kuzuru nchi inayokumbwa na mliipuko wa Zika.