Je, Gbagbo ni nani?

Haki miliki ya picha
Image caption Laurent Gbagbo

1945.Bw.Gbagbo alizaliwa katika familia ya kikatoliki karibu na Gagnoa,eneo lililo katikati magharibi mwa taifa hilo ambapo Cocoa hukuzwa terehe 31 mwezi May

''Cicero'', kwa jina la utani kutokana na kupenda kwake lugha za kilatin wakati alipokuwa shule na anamiliki shahada ya uzamifu katika historia.

1971.Alianza kazi kama muhadhiri wa chuo kikuu,na baadaye alihudumia kifungo cha miaka 2 jela mwaka kwa kufunza mapinduzi.

1980. Alishiriki katika uanaharakti wa vyama vya wafanyikazi miongoni mwa wasomi.

Alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpatia changamoto rais wa kwanza wa taifa hilo miaka ya 80,baada ya rais huyo aliyehudumu kwa kipindi cha mda mrefu kuruhusu vyama vingi vya kisiasa.

1982. alienda mafichoni mjini Paris,na kurudi miaka sita baadaye ambapo alijiunga na chama cha kisiasa cha FPI.

Akihudumu kama kiongozi wa upinzani alihudumia vifungo jela na kukosana na serikali.

2000.Baada ya miaka 20 ya upinzani,alichukua mamlaka wakati jaribio la kiongozi wa jeshi Robert Guei kutaka kufanya udanganyifu katika uchaguzi liliposhindwa na maandamano ya raia katika mji mkuu wa Abidjan.

Baada ya kuchaguliwa bwana Gbagbo alisema kwamba hataendelea na sera za uongozi uliokuwepo akisema sio muhimu kuweka picha za raia katika maeneo ya uma na afisini.

Pia alisema kwamba vyombo vya habari havitalazimika kutaja jina la rais katika kila vipindi vyote vya habari.Lakini alipokuwa mamlakani habari nyingi ziliangazia mambo aliyofanya Gbagbo.

Anajulikana kwa kuwa mtu mwenye hasira hususan dhidi ya waandishi wenye kiburi,lakini pia anajulikana kwa kicheko chake na anaposalimiana na mkono.

2011.Mnamo mwezi Aprili ,bw. Gbagbo alilazimishwa kutoka afisini ,alipokamatwa ndani ya shimo ndani ya jumba la rais na wanajeshi wa umoja wa mataifa na wale wa Ufaransa waliokuwa wakimuunga mkono mpinzani wake Alassane Outtara ,ambaye alibainika kimataifa kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika miezi mitano iliopita.

Gbagbo baadaye alihamishwa hadi katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC mjini The Hague,na ni kiongoza wa kwanza wa taifa kushtakiwa na mgogoro uliotokea ambapo takriban watu 3000 waliuawa.

Mkewe Simon ,alikuwa mwanasiasa wa kivyake na wengi walimuona kuwa mshinikizi mkubwa wa serikali ya Gbagbo,ambapo alimzuia mumewe kuachilia mamlaka.Pia yeye yuko jela.

Mahakama moja nchini Ivory Coast ilimhukumu kifungo cha miaka 20 kwa jukumu lake la ghasia hizo za baada ya uchaguzi wa 2010.

Mahakama ya ICC ilitoa agizo la kukamatwa kwa Simone Gbagbo,lakini agizo hilo lilitupiliwa mbali na serikali ya Ivory Coast.

Yeye mwenyewe hupenda kutabasamu na kucheka na ni mtu mzungumzaji anayetumia sana misemo ya Ivory Coast ya maisha ya kawaida.

Hudaiwa kupenda muziki,kupiga gita na chakula kizuri.