Ujerumani yabana watafutao hifadhi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sigmar Gabriel Makamu Kansela wa Ujerumani

Muungano wa serikali ya ujeramani umetoa maelekezo ya namna gani mipango ifanyike ili kubana sheria za wanaotafuta makazi baada ya kuingia kwa zaidi ya wahamiaji milioni moja mwaka jana.

Makamu kansela wa Ujerumani, Sigmar Gabriel amesema wale walioingia kwa vikwazo hawataruhusiwa kuleta ndugu zao nchini Ujeremani kwa kipindi cha miaka miwili.

Kansela huyo alisema nchi tatu ;Algeria,Morocco na Tunisia zitakuwa salama na mataifa hayo yanategemea kuwa na uwezo wa kupokea wakimbizi.

vilevile kuna hatua nyinginge mpya ambazo zitatumika ili kuharakisha kuwaondoa waliokosa hifadhi.