Mexico yampa bintiye 'El Chapo' hati miliki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Joaquin "El Chapo" Guzman

Afisi ya serikali ya Mexico inayosimamia utoaji wa leseni za hati miliki imeruhusu mwanawe kiongozi wa genge la Sinaola aliyekamatwa majuzi Joaquin "El Chapo" Guzman, hati miliki ya kutumia jina lake la utani kama nembo ya kibiashara .

Alejandrina Guzman amepata idhini ya kutumia "El Chapo" ambayo ni tafsiri ya mtu mfupi kuuza bidhaa kama vile saa begi za wanawake miavuli mbali na vipuli na herini.

Afisi hiyo ya kutoa hati miliki imesema kuwa "El Chapo" sio tusi na hivyo haitawaudhi wanunuzi.

"El Chapo" mwenyewe alikamatwa majuzi baada ya kuutamausha ulimwengu kwa uwezo wake mkubwa wa kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali nchini Mexico.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption "El Chapo" mwenyewe alikamatwa majuzi baada ya kuutamausha ulimwengu kwa uwezo wake mkubwa wa kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali nchini Mexico.

Kwa sasa kiongozi huyo wa genge la Sinaola amerejeshwa anatarajiwa kupelekwa marekani kujibu mashtaka dhidi yake.

Hata hivyo muda mchache baada ya raia wa Mexico kupata habari kuhusu hatua hiyo ya serikali ya Mexico, kuhalalisha hati miliki ya msichana huyo wa Guzman, Alejandrina, shinikizo limeibuka la kuitaka serikali kuifutilia mbali leseni hiyo.

Gazeti moja nchini humo Milenio' lilichapisha habari hiyo yapata miaka 5 baada ya serikali kuidhinisha bi Alejandrina, kutumia nembo ya "El Chapo" katika bidhaa za kibiashara.