Kenya na Nigeria kushirikiana dhidi ya ugaidi

Haki miliki ya picha NTV
Image caption Kenya na Nigeria zimeafikiana kuungana katika kukabiliana dhidi ya ugaidi.

Kenya na Nigeria zimeafikiana kuungana katika kukabiliana dhidi ya ugaidi.

Wakizungumza katika ikulu ya Nairobi , Rais wa Nigeria Muhammud Buhari pamoja na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta wamesema kuwa nchi hizo mbili zitashirkiana katika kupambana na ugaidi.

Viongozi hao wamesema kuwa nchi zao zimeumizwa na kuhangaishwa na magaidi kwa muda mrefu.

Rais Buhari amesema Nigeria imehangaishwa sana na wapiganaji wa Boko Haram nayo Kenya ikishambiliwa mara kwa mara na wapiganaji wa Al shabaab kutoka Somalia.

"Magaidi wamekuwa wakibadili mbinu na mahusiano na hata kuungana na makundi mengine.

Image caption Wanajeshi wakenya wameuawa majuzi na Al shabab katika kambi ya el ade

''Haya yote ni katika jitihada za kujiongezea uwezo wao wa kuwaumiza watu wasiokuwa na hatia yeyote''.

''Kwahiyo tukitaka kushinda vita hivi vya ugaidi nilazima nasi tuje na mbinu na mikakati mipya". alisema rais Kenyatta.

Rais huyo wa Nigeria amesema kwa wakati huu hakuna nchi inayoweza kujigamba kwamba haiwezi kushambuliwa na magaidi.

kutokana na hili Buhari amezitaka jamii ya kimataifa kushirikiana katika kupambanana na tatizo la ugaidi.

"Jamii yote ya kimataifa ni sharti ishirikiane kwa karibu zaidi na hasa katika kugawana na kupashana habari za kijasusi.

''Pia kuna haja kubwa ya kuleta pamoja raslimali ili kukabiliana na janga hili.''

''Majeshi na walinda usalama wetu ni lazima wawezeswhe vilivyo na kutiwa motisha ili waweza kukabiliana na ugaidi."Alisema Kiongozi huyo wa Nigeria ambaye yuko Kenya katika ziara ya siku tatu.

Image caption Rais Buhari amesema Nigeria imehangaishwa sana na wapiganaji wa Boko Haram

Apowasili tu nchini Kenya alijiunga na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta kuhudhuria sherehe maalum za kidini kuomboleza wanajeshi wa Kenya waliouwawa katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa al shabaab katika kambi ya AMISOM iliyokuwa ni makao ya wanajeshi wa Kenya huko el Ade.

Tatizo jengine ni mafunzo ya kidini yenye itikadi kali hasa miongoni mwa waislamu.

Rais Buhari amesema hilo pamoja na mafunzo yenye kuchochea vujo na mashambulizi ni lazima yakabiliwe.

"Mafunzo ya kidini yenye itikadi kali pamoja na uchocheaji wa fujo na mashambulizi ni mambo ambayo yanasambaa katika bara la Afrika.

Hali hii lazima ikomeshwa tukitumia mbinu za kisasa. Kutokana na hili nchi zetu lazima zisaidiwe na kuungwa mkono katika kupambana na hali hii ya uchocheaji mashambulizi kwa kutumia mafunzo ya kidini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kenya imeshambiliwa mara kwa mara na wapiganaji wa Al shabaab kutoka Somalia.

Ni lazima tukabiliane na mafunzo ya kidini yenye itikadi kali yanayosambazwa na watu wenye itikadi kali za kidini kwa kutoa mafunzo na ujumbe sahihi na usio na makali na kuwashauri watu kuvumiliana na kuwa na subra".

Kwa Upande wake rais wa Kenya ,Uhuru Kenyatta amesema maendeleo ya nchi hayawezi kufikiwa bila ya kuweko kwa usalama na amani nchini.

Kenyatta amekiri kuwa ugaidi umekuwa ni tatizo kubwa sana nchini Kenya.

Uhuru Kenyatta amesema kuwa Umoja wa Afrika unafanya kazi kubwa sana kuijenga upya Somalia na kuhakikisha inarudi hali yake ya kawaida.

Rais huyo wa Kenya amesema Kenya haitatoka Somalia hadi watakapowaangamiza magaidi..