Wakimbizi wa Morocco kurudishwa nyumbani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi

Morocco inasema kuwa itawarudisha nyumbani raia wake ambao wameshindwa kupata kibali cha ukimbizi nchini Ujerumani.

Taarifa kutoka taifa hilo zinasema kuwa mfalme Mohammed alifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na kansela wa Ujerumani Angela Merkel siku ya Jumatano.

Taarifa hiyo imesema kuwa mataifa hayo mawili yalikubaliana kuangazia visa vya wale wanaoishi Ujerumani bila vibali na kwamba watarudishwa nchini Morocco bila kupoteza wakati.

Maelfu ya wahamiaji na wakimbizi kutoka kaskazini mwa Afrika wamejaribu kuingia Ulaya katika siku za hivi karibuni.