Kenya: Wawili kujibu mashtaka ya mauaji ya watu 60

Mpeketoni Haki miliki ya picha ODPP
Image caption Upande wa mashtaka uliita mashahidi zaidi ya thelathini

Mahakama Kuu mjini Mombasa imeamua kwamba washukiwa wawili walioshtakiwa mauaji ya watu 60 eneo la Mpeketoni miaka miwili iliyopita wana kesi ya kujibu.

Jaji Martin Muya amesema upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka wawili hao.

Bw Diana Salim Suleiman na Mahadi Suleiman Mahadi ajulikanaye sana kama Jesus wanadaiwa kuhusika katika uvamizi uliopelekea kuuawa kwa watu 60 mwezi Juni mwaka 2014 katika vijiji vya Mpeketoni na Kaisairi, Kaunti ya Lamu.

Wanakabiliwa na mashtaka 60 ya mauaji.

Upande wa mashtaka uliowasilisha mashahidi takriban 30 kutoa ushahidi dhidi ya wawili hao.