Waziri ajiuzulu kwa madai ya ufisadi Japan

Haki miliki ya picha EPA
Image caption waziri Akira Amari kushoto

Waziri wa uchumi nchini Japan Akira Amari amesema anajiuzulu kutokana na madai ya ufisadi.

Bwana Amari alitoa tangazo hilo bila kutarajiwa katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi.

Kadhalika alikanusha kupokea hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi kama ilivyodaiwa na jarida moja la Japan.

Hatua hiyo itachukuliwa kama pigo kubwa kwa waziri mkuu Shinzo Abe.

Bwana Amari alitarajiwa kusafiri hadi New Zealand wiki ijayo kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya mataifa ya ng'ambo ya pili ya bahari ya Pacific.