Tenis: Serena Williams anusia rekodi mpya

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Serena Williams anusia rekodi mpya

Mchezaji anayeorodheshwa nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams yuko mbioni kuandikisha rekodi ya kuwa mwanamke aliyewahi kushinda michuano mingi zaidi duniani endapo atashinda fainali ya wanawake ya mchuano wa Australian Grand Slam siku ya jumamosi.

Mmarekani huyo alijiweka katika nafasi nzuri ya kuweka historia baada ya kumbwaga Agnieszka Radwanska seti mbili kwa nunge za alama 6-0, 6-4 katika hatua ya nusu fainali .

Endapo Williams ataibuka mshindi dhidi ya mchezaji anayeorodheshwa katika nafasi ya 7 duniani Angelique Kerber, basi atakuwa ameshinda mashindano 22 makubwa ya tenisi ya wazi na kufikia rekodi iliyowekwa na Steffi Graf aliposhinda mataji 22.

Vilevile atakuwa amempiku graf na kuwa mwanamke wa pili baada ya Margaret Court aliyeandikisha rekodi ya kushinda mataji 24.

''kwa hakika mimi sitafuti rekodi, mimi natafuta kushinda taji la mwaka huu.

umeshasahau mwaka uliopita kila mtu alikuwa akiniuliza swali naskiaje kuwa nimesalia na rekodi moja tu kabla ya kufikia rekodi ya kuwa mwanamke bora zaidi katika historia ya tenis ?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Williams kuchuana na Angelique Kerber katika fainali ya Australian Open

Nitaizuia ,,,bila shaka sitaitilia maanani hadi baada ya mechi.'' Alisema Williams katika mkutano na waandishi wahabari.

Mpinzani wake Kerber alimtamausha muingereza Johanna Konta katika hatua ya nusu fainali aliomlaza seti mbili kwa nunge za alama 7-5, 6-2 na kujikatia tikiti ya fainali yake ya kwanza ya Grand slam.

Licha ya kushindwa Konta ndiye aliyekuwa mwanamke wa kwanza Muingereza kufuzu kwa nusu fainali ya mchuano kama huo tangu mwaka wa 1983 .

Kwa upande wake Kerber anatafuta ushindi wake wa pili dhidi ya Williams tangu mwaka wa 2012