Rwanda inaongoza kwa kunyonyesha watoto duniani

Image caption Mtoto anayenyonya

Shirikisho la afya duniani WHO limetoa takwimu mpya kuhusu umuhimu wa kunyonyesha duniani huku Rwanda ikiwa na viwango vya juu vya asilimia 85.

Miongoni mwa mataifa yenye viwango vya chini vya unyonyeshaji ni Uingereza ambapo ni asilimia 1 pekee ya akina mama wanaowanyonyesha wanao kwa kpindi cha miezi 6 ya kwanza.

Katika ripoti,watafiti wanasema kuwa vifo vya zaidi ya watoto 800,000 vinaweza kukingwa kila mwaka kwa kuimarisha viwango hivyo.

Wanasema kuwa hatua hiyo hupunguza visa vya saratani ya matiti miongoni mwa watoto.

Utafiti huo uliochapishwa na jarida la afya la Lancet unaonyesha ni mwanamke mmoja tu kati ya 200 ama asilimia 0.5 wanaondelea kunyonyesha baada ya mwaka.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mama anayenyonyesha

Hiyo ni tofauti na asilimia 23 ya Ujerumani ,56 ya Brazil na 99 ya Senegal.

Watafiti wamesema kuwa sio kweli kwamba unyonyeshaji watoto husaidia pekee katika mataifa masikini.

Nchini Uingereza asilimia 81 ya akina mama walijaribu kuwanyonyesha watoto katika wakati mmoja lakini ni asilimia 34 walioendelea kunyonyesha katika mwezi wa sita na 12.

Nchini Marekani asilimia 79 walianza asilimia 49 wakiendelea kunyonyesha huku asilimia 27 wakinyonyesha baada ya mwaka mmoja.

Ni rekodi mbaya duniani ,unyonyeshaji wa watoto hufanyika sana katika mataifa yanayoendelea,lakini takwimu nchini Uingereza ziko nyuma ikilinganishwa na mataifa mengine Ulaya.

Wanawake nchini Uingereza wanashauriwa kuwanyonyesha wanao na maziwa ya matiti kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza na baadaye wachanganye maziwa hayo na vyakula vyengine,lakini hawaelezwi ni wakati gani wanapofaa kumaliza kunyonyesha.

Image caption Wanawake wa Afrika wanaonyonyesha

Unyonyeshaji watoto ni mzuri kwa afya ya mtoto na hupunguza hatari ya matiti na saratani ya ovari.

Profesa Cesar Victora kutoka nchini Brazil amesema kuwa kuna uvumi unaoenea kwamba maziwa ya matiti huwasaidia watoto kutoka mataifa masikini.

''Hiyo si kweli kwani kazi yetu inaonyesha wazi kwamba maziwa ya matiti huokoa maisha na fedha katika mataifa yote,tajiri na masikini''.

Ripoti hiyo ya lancet imesema kuwa unyonyeshaji wa watoto katika mataifa yalioendelea hupunguza hatari ya kufariki kwa watoto kwa zaidi ya thuluthi moja.