Rushwa: Mkuu wa jeshi wa zamani ahojiwa Nigeria

Adesola Amosu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Adesola Amosu amezuiliwa na maafisa wa kupambana na ufisadi tangu Jumatano

Mkuu wa zamani wa jeshi la wanahewa nchini Nigeria amehojiwa na tume ya kupambana na ufisadi nchini humo kuhusiana na kupotea kwa pesa za jeshi.

Shirika la habari la AFP, likinukuu mdokezi katika tume hiyo ya kukabiliana na ufisadi, linasema afisa huyo, Adesola Amosu, anachunguzwa kuhusiana na matumizi mabaya ya pesa zilizotengewa jeshi.

Mdokezi huyo amesema Amosu amekuwa akihojiwa na maafisa wa tume hiyo tangu Jumatano.

Yeye ni miongoni mwa wanajeshi 20 wa zamani wa jeshi, baadhi yao maafisa wa ngazi ya juu ambao, Rais Muhammadu Buhari aliagiza wachunguzwe kuhusiana na ulaghai wakati wa ununuzi wa silaha za kutumiwa na jeshi.