Vitufe vipya vya maoni kuongezwa Facebook

Vitufe
Image caption Vitufe vitano vitaongezwa karibuni

Facebook inapanga kupanua kitufe cha Kupenda kwenye mtandao wake wa kijamii na kuwezesha watu kutumia picha tano mpya za kutolea maoni au kwa Kiingereza Reactions.

Mwanzilishi na Mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg amesema watu 1.5 bilioni wanaotumia mtandao huo wataweza kutumia vitufe hivyo vipya “karibuni”.

Kwa sasa, vitufe hivyo vipya vya picha vya kutolea maoni ambavyo ni "penda", "haha", "wow", "yahuzunisha" na"yakasirisha" vinafanyiwa majaribio katika mataifa kadha.

Kila maoni yanaendana na picha ya sura ya kibonzo (emoji) ambayo itakuwa ikitokea chini ya ujumbe au kitu kilichopakiwa na mtu mtandaoni.

Watu watakuwa wakibofya na kinatokea chini ya ujumbe.

Wakati wa kufanyiwa majaribio, kulikuwa na kitufe kingine kilichoitwa "yay" ambacho hakitatumika tena kwani Facebook wanasema watu hawakuelewa matumizi yake.

Kwa muda mrefu, watu walizoea kutumia kitufe cha ‘penda’ hadi majuzi kitufe cha ‘kutopenda’ kilipoongezwa.