Japan yapunguza viwango vya riba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Japan

Benki Kuu ya Japan imetangaza kupunguza zaidi viwango vya riba kama hatua ya kuuchepua uchumi wa nchi.

Wateja walio na akaunti za benki wataanza kupata faida ya riba chini ya asili mia sufuri, hivyo salio lolote kwenye benki litatozwa ada.

Hii ndio mara ya kwanza benki kuu ya Japan imefanyia mageuzi viwango vya riba kwa zaidi ya miaka mitano.

Tangazo hilo limepokelewa vyema na soko la hisa la Tokyo ambapo bei ya hisa ilipanda kwa zaidi ya asili mia mbili.