Nemanja Vidic astaafu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Nemanja Vidic

Aliyekuwa beki matata na nahodha wa kilabu ya Manchester United Nemanja Vidic ametangaza kustaafu katika soka ya kulipwa.

Raia huyo wa Serbia ambaye alishinda mechi tano za ligi ya Uingereza na kombe la kilabu bingwa Ulaya katika miaka yake minane akiichezea Manchester United amesema kuwa majeraha yamemlazimu kustaafu.

Vidic,mwenye umri wa miaka 34,aliondoka katika kilabu ya Inter Milan baada ya makubaliano mnamo mwezi Januari baada ya kushindwa kushiriki katika mechi za Serie A msimu huu.

''Ni wakati kwa mimi kustaafu,aliuambia mtandao wa manUtd.com.

Vidic alijiunga na Inter Milan kwa uhamisho wa bila malipo mnamo mwezi Julai 2014 na aliichezea the Azzuris mara 28 katika kampeni yake ya kwanza,lakini ameshindwa kukichezea kikosi cha Robertto Mancini msimu huu kutokana na jeraha la mguu.