Marekani:Korea Kaskazini kurusha roketi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Roketi

Korea Kaskazini huenda inajiandaa kurusha roketi, maafisa wa Marekani wamesema kufuatia vitendo vingi vinavyofanywa katika kituo cha satelite cha Sohae.

Afisa mmoja alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba uzinduzi huo huenda ukawa wa Satelite ama kituo cha angani.

Lakini iwapo hakuna lililotangazwa huenda ni kombora,aliongezea.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo baraza la usalama la umoja wa mataifa linajadili vikwazo vipya dhidi ya Korea kaskazini baada ya kufanya jaribio la nne la silaha ya Nuklia mnamo tarehe 6 Januari.

Image caption Roketi

Pyongyang imesema kuwa ilifanikiwa kujaribu bomu la maji ,lakini wataalam wa zana za nuklia walihoji madai hayo wakisema kuwa mlipuko wake haukuwa mkubwa.

Siku ya Alhamisi asubuhi,chombo cha habari cha Kyodo nchini humo kiliripoti kwamba maafisa wa Japan walikuwa na wasiwasi kuhusu vitendo vunavyofanyika katika katika kituo hicho cha satelite kinachojulikana kama Tongchang-ri.