Walimu 4 kati ya 10 hushambuliwa na wanafunzi

Image caption Mwalimu aliyeshambuliwa na wanafunzi

Walimu wanne kati ya 10 wamepigwa ama hata kushambuliwa na wanafunzi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita,utafiti umesema.

Kati ya walimu 1,250 waliofanyiwa utafiti na muungano wa walimu na wahadhiri ATL nchini Uingereza,asilimia 77 wamesema kuwa walisukumwa,kupigwa kumbo huku nusu yao wakisema walipigwa ama hata kurushiwa kitu.

Tisa kati ya walimu 10 walikabiliana na tabia hiyo mbaya kama vile kuapa mungu ama hata kupiga kelele katika kipindi cha mwaka mmoja.

Serikali imesema kuwa walimu sasa wana mamlaka zaidi dhidi ya wanafunzi hao na swala la utumizi wa nguvu limetatuliwa.

Hatahivyo asilimia 45 ya walimu waliohojiwa nchini Uingereza,Wales, na Ireland Kaskazini wamesema kuwa wanahisi tabia za wanafunzi zimezidi kuwa mbaya katika kipindi cha miaka miwili iliopita.

Walimu wa Uskochi hawakushirikishwa katika utafiti huo.

Walimu wamesema kwamba ghasia hizo husababishwa na mambo kadhaa.

Ukosefu wa mpaka nyumbani kati ya wazazi na wanafunzi umetajwa kama sababu kuu ya utovu wa nidhamu.

Asilimia 78 imesababishwa na mhemuko pamoja na matatizo ya tabia huku wengine wakisema kuwa imesababishwa na matatizo ya kiafya ya ubongo wa mtu.

Vilevile thuluthi mbili ya walimu wamehoji kwamba wanafunzi walikuwa chini ya shinikizo zaidi ya miaka miwili iliopita.