Wanajeshi kukabiliana na kunguni Uganda

Image caption Kunguni Uganda

Wanajeshi wa Uganda watakwenda kila nyumba kunyunyiza dawa ya kuangamiza kunguni ikiwa ni miongoni mwa shughuli zao za kijamii wakati wa kuadhimisha wiki ya jeshi.

Kulingana na gazeti la the New Vision, wadudu hao wamejazana katika kijiji kimoja cha mabanda nje ya mji wa Kampala, mwandishi wa BBC Patience Atuhaire anasema.

Wiki hiyo ya jeshi ambayo huadhimishwa kila mwaka inalipa fursa jeshi kushiriki katika shughuli za kijamii kama vile kufagia barabara na kufungua mitaru ya maji taka.

Ripota wetu amesema kuwa ni miongoni mwa shughuli za jeshi ili kujiweka karibu na raia wa Uganda.