Chad yachukua uenyekiti wa AU

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Chad Idris Deby

Rais wa Chad Iddris Deby ndio mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika baada yakuchukua mahala pake mwenyekiti anayeondoka rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Lakini ni Mugabe aliyetawala katika vyombo vya habari akitaka Umoja wa mataifa kufanyiwa marekebisho.

Akilitaja baraza la usalama la umoja wa mataifa,Mugabe amesema kuwa viongozi wa Afrika wana haki ya kupewa mamlaka zaidi katika maamuzi yanayofanywa katika baraza hilo.

Mugabe alikuwa akizungumza katika Mkutano wa umoja wa Afrika unaoendelea mjini Addis Ababa Ethiopia.