Wanajeshi waliodhulumu watoto CAR watajwa

Haki miliki ya picha f
Image caption Wanajeshi

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umeweka wazi uraia wa wanajeshi wa kulinda amani wanaoshtumiwa kuwa wamekuwa wakiwadhulumu watoto kingono Jamhuri ya Afrika ya kati.

Washukiwa hao ni raia wa Bangladesh, the DRC, Niger na Senegal.

Akihutubia wanahabari mjini New York, afisa mkuu wa UN Anthony Banbury karibu atokwe na machozi wakati alipotangaza kesi za hivi karibuni za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.

Mwezi ulopita, jopo huru lilikashifu jibu la UN kuhusu madai hayo kama yenye makosa makubwa.