Barua za Clinton zatajwa kuwa na 'siri kali'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hillary Clinton

Timu ya kampeni za urais za Hillary Clinton imeikashifu vikali wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani kwa kuzuia kutolewa kwa baadhi ya barua pepe za Clinton zenye siri, hata baada ya kutangazwa kuwa si za siri kali

Msemaji wa timu ya kampeni za bi Clinton Brian Fallon ametaja hatua hiyo kama isiyofaa.

Wizara ya maswala ya kigeni imesema kuwa barua pepe hizo zimetangazwa tena kuwa za siri kali baada ya ombi la maafisa wa ujasusi.

Utata kuhusu matumizi ya barua pepe za binafsi wakati bi clinton alipokiwa waziri wa mambo ya nje umekuwa ukitatiza kampeni zake za kupeperusha bendera ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa Marekani mwakani.