Mugabe alionya baraza la usalama la UN

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mugabe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelitaka baraza la usalama la umoja wa Mataifa kufanyiwa marekebisho.

Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Afrika unaondelea mjini Addis Ababa Ethiopia,Mugabe amesema kuwa viongozi wa Afrika wana haki ya kupewa mamlaka zaidi katika maamuzi yanayofanywa katika baraza hilo.

Huku akishangiliwa na viongozi wenzake wa Afrika,rais huyo mwenye umri wa miaka 91, ametaka bara la Afrika kupewa viti viwili vya kudumu katika baraza hilo la usalama.

Mugabe amesema kuwa ombi hilo sio kubwa sana kutoka kwa bara ambalo lina zaidi ya wanachama 50 katika baraza hilo.

Amesema kuwa Bara la Afrika haliwezi kuwa na uanachama wa mda katika baraza hilo,huku akionya kujitoa kwa bara hili iwapo mahitaji yao hayatasikizwa.

Haki miliki ya picha un.org
Image caption Baraza la usalama la UN

Amelilaumu baraza la umoja wa kimataifa kwa kuendeshwa kiukubwa.MUgabe ameonya kwamba Baraza hilo la umoja wa Kimataifa litaendelea kudumu kupitia kufanya usawa miongoni mwa wanachama wake.

Hatahivyo aliunga mkono juhudi za katibu mkuu wa umoja wa kimataifa Ban Ki Moon kwa kuangazia maswala ya bara hili.